Afrika Kusini yasherehekea miaka 25 ya uhusiano wa kidiplomasia na China
2023-01-02 08:50:48| CRI

Afrika Kusini jana jumapili imesherehekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na China.

Taarifa iliyotolewa katika tovuti ya Idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano ya nchini humo imesema, katika kipindi hicho cha miaka 25, nchi hizo mbili zimeimarisha kwa kina uhusiano wa pande mbili, ambao umekuzwa na kufikia ngazi ya Uhusiano wa Kina wa Kimkakati na kuimarishwa na Mradi wa Miaka 10 wa Ushirikiano wa Kimkakati wa mwaka 2020 – 2029.

Taarifa hiyo imesema, mawasiliano ya mara kwa mara kati ya Afrika Kusini na China yanafanyika katika ngazi mbalimbali, ikiwemo ziara za viongozi wa ngazi za juu na ushirikiano kati ya wizara mbalimbali za serikali za nchi hizo mbili.

Taarifa hiyo pia imesema, pande hizo mbili ziko tayari kutafiti maeneo mengine ya ushirikiano wa kunufaishana, ukuaji wa uchumi, na ustawi wa mataifa hayo mawili.