Huawei yajitahidi kuendeleza vipaji vya ICT na uvumbuzi wa mfumo wa ikolojia nchini Ethiopia
2023-01-02 08:51:34| CRI

Kampuni ya mawasiliano ya China Huawei tawi la Ethiopia imesema zaidi ya wanafunzi 60 nchini Ethiopia wameshiriki katika shindano la teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa mwaka 2022-2023, linalolenga kuendeleza vipaji vya TEHAMA na uvumbuzi katika mfumo wa ikolojia.

Shindano hilo lilifanyika jumatano iliyopita katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, na kuhudhuriwa na wanafunzi 63 kutoka zaidi ya vyuo vikuu 30 vya serikali na binafsi.

Kampuni hiyo imesema, lengo la shindano hilo ni kuwapatia wanafunzi mazingira salama, ambako wanaweza kushindana na kubadilishana maoni, na hivyo kuboresha ujuzi wao katika TEHAMA na kuongeza uwezo wao wa uvumbuzi kwa kutumia teknolojia na majukwaa mapya.