Watu wanne wafariki katika ajali ya kugongana kwa helikopta
2023-01-03 08:20:11| cri


 

     Polisi wa Queensland, Australia wamesema, watu wanne wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya helikopta mbili kugongana jana.

Polisi wamesema, jana alasiri, helikopta iliyokuwa ikiruka iligongana na helikopta nyingine iliyokuwa ikitua katika eneo la pwani ya Queensland.

Habari zinasema, kulikuwa na watu 13 kwenye helikopta hizo mbili, na majeruhi wamepelekwa hospitali ya karibu kwa ajili ya matibabu.