Kenya yazindua mpango wa kuongeza megawati 3,000 za umeme wa kijani katika gridi ya taifa
2023-01-06 08:27:56| CRI

Shirika la Kuzalisha Umeme nchini Kenya (KenGen) limetangaza mpango wa kuongeza megawati 3,000 za umeme wa kijani kwenye gridi ya taifa katika miaka 10 ijayo. 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Abraham Serem amesema, mkakati huo utaongozwa kwa matumizi ya umeme wa nishati ya joto la chini ya ardhi na umeme wa nishati ya maji ili kutuliza vyanzo vya nishati nchini humo.

Ameongeza kuwa, ujenzi wa kituo cha kuzalisha megawati 280 za umeme kwa nishati ya joto la chini ya ardhi katika eneo la Olkaria, na ujenzi wa kituo cha kuzalisha megawati 25 za umeme huko Eburru katika mkoa wa Bonde la Ufa utaanza mara baada ya kupata vibali vinavyotakiwa.