Rais wa Russia aliamuru jeshi kusitisha vita kwa siku moja na nusu wakati wa sikukuu ya Krismasi ya Waorthodox
2023-01-06 08:26:14| cri

Rais wa Russia Vladimir Putin ameliamuru jeshi la nchi hiyo kusitisha vita na Ukraine kuanzia saa sita usiku wa tarehe 6 kwa saa za Russia hadi saa sita usiku wa tarehe 7, ili kupisha Sikukuu ya Krismasi kwa watu wa dhehebu la Orthodox.

Rais Putin amesema hatua hiyo inafuatia pendekezo lililotolewa na uongozi wa dhehebu hilo nchini Russia. Pia rais Putin ametoa wito kwa Ukraine kusitisha vita ili kuwapa waumini fursa ya kufanya shughuli za kidini wakati wa kipindi cha Krismasi ya Waorthodox.