Usambazaji wa misaada waboreka katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia
2023-01-06 08:28:43| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, usambazaji wa misaada katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia umeboreshwa, huku baadhi ya maeneo yakishindwa kufikiwa na misaada hiyo.

Amesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeripoti kuwa, kati ya mwezi Novemba na mwisho wa mwezi Desemba, zaidi ya malori 3,000 yaliyobeba chakula na vifaa vingine ikiwemo maji yaliingia kwenye eneo la kaskazini mwa Ethiopia kupitia barabara na kwa kutumia ndege.

Ofisi hiyo imeonya kuwa, kiwango cha utapiamlo kimeendelea kuwa cha juu, huku moja ya tatu ya watoto waliopimwa mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana wakikutwa na utapiamlo mkali.