Rais Xi asisitiza haja ya kuhimiza Chama kujisimamia chenyewe kikamilifu
2023-01-10 08:38:45| CRI

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Bw. Xi Jinping amesisitiza haja ya kuendeleza juhudi za kuhimiza Chama kujisimamia kikamilifu na kwa hatua kali, na kuhakikisha utekelezaji wa maamuzi na mipango iliyowekwa katika Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

Bw. Xi ambaye pia ni Rais wa China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Jeshi, alitoa kauli hiyo alipohutubia kikao cha pili cha Kamati Kuu ya 20 ya CPC ya Ukaguzi wa Nidhamu (CCDI).

Bw. Xi amesema Kwa ajili ya maslahi ya Chama kwenye utawala wa muda mrefu, ustawi na utulivu wa kudumu wa nchi na furaha ya wananchi, Chama kujisimamia kwa pande zote na kwa hatua kali kunapaswa kupewa kipaumbele na kuwa mkakati wa muda mrefu wa Chama.