Kikundi cha madaktari wa China chachangia vifaa tiba kwa Hospitali ya Gabon
2023-01-11 09:02:28| CRI

Kikundi cha madaktari wa China nchini Gabon kimetoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali ya Ushirikiano kati ya China na Gabon mjini Libreville, ili kuimarisha utoaji wa huduma.

Mkuu wa timu ya madaktari wa China Bw. Zhao Zhizheng amesema msaada huo ni pamoja na vifaa tiba na dawa zinazohitajika sana, kama sindano za akupancha na plasta.

Bw. Zhao amesema hospitali hiyo imekuwa na upungufu wa vifaa tiba kwa muda mrefu, lakini amesisitiza kuwa kikundi chake kitatekeleza majukumu yake.

Mkuu wa Hospitali hiyo Bw. Gisele Kouanga ameshukuru msaada huo na kuutaja kuwa ni ishara ya ukarimu, na kupongeza uungaji mkono uliotolewa na madaktari wa China nchini Gabon katika miongo miwili iliyopita.

Amesema matibabu ya jadi ya China na hasa tiba ya Akupancha, yanapendwa sana na watu wa Gabon.