UNICEF yahitaji dola milioni 272 kuwasaidia Wasomali milioni 3 mwaka huu
2023-01-13 08:57:54| CRI

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linahitaji dola za kimarekani milioni 272.3 ili kutoa huduma za kibinadamu kwa watu milioni 3, wakiwemo watoto milioni 2, nchini Somalia kwa mwaka huu.

Shirika hilo limesema fedha hizo zitaliwezesha kutoa huduma muhimu hasa kwenye maeneo yasiyofikika kirahisi, na pia zitalisaidia kuimarisha uongozi wake kwenye kazi za uratibu.

Kwa mujibu wa UNICEF watoto milioni 1.8 chini ya miaka mitano nchini Somalia wanakadiriwa kukonda kabla ya mwezi Julai mwaka huu, kutokana na ukame mkali, migogoro na kupanda kwa bei ya chakula.