UM: Raia 27 wauawa mashariki mwa DRC wiki hii
2023-01-13 09:24:25| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema makundi ya kisilaha yaliyoko katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yamewaua raia wasiopungua 27 nchini humo wiki hii.

Amesema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo (MONUSCO), hali katika eneo la Djugu imekuwa mbaya baada ya kushambuliwa wikiendi iliyopita na wapiganaji kutoka muungano wa makundi ya kisilaha unaojulikana kuwa CODECO.

Pia amesema walinzi wa amani wa UM wanafanya doria huko Roe-Drodo kulisaidia jeshi la DRC kulinda raia wake na wamewasindikiza baadhi ya raia kurudi kwenye kambi ya wakimbizi huko Roe.