Rais wa Gabon akutana na waziri wa mambo ya nje wa China
2023-01-13 08:56:50| CRI

Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon jana mjini Libreville alikutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang ambaye yuko ziarani nchini humo.

Bw. Qin amefikisha salamu za Rais Xi Jinping kwa Rais Ondimba, akisema uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ambao umejengwa kwa pamoja na viongozi waasisi wa pande hizo mbili, umepitia majaribu ya wakati na kuendelea kuwa imara.

Amesema China iko tayari kufanya kazi na Gabon katika kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuimarisha hali ya kuaminiana kimkakati, kuendeleza ushirikiano halisi na kuinua uhusiano kati ya China na Gabon hadi kwenye ngazi mpya.

Rais Ondimba amemtaka Bw. Qin kufikisha salamu zake kwa Rais Xi Jinping, akiishukuru China kutokana na uungaji mkono wake endelevu na thabiti kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya Gabon.

Amesema urafiki kati ya Gabon na China umezidi kuimarika wakati nchi hizo mbili zinahimiza maendeleo ya pamoja na kulinda maslahi ya pamoja.