Waziri wa mambo ya nje wa China na Mkuu wa AL watoa wito wa kutekeleza haraka matokeo ya Mkutano wa China na Nchi za Kiarabu
2023-01-16 14:05:34| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) Ahmed Aboul Gheit Jumapili walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa China na Nchi za Kiarabu.

Kwenye mkutano wao mjini Cairo, Misri, Qin alisifu kuitishwa kwa Mkutano huo mwezi uliopita kwa mafanikio kama "hatua muhimu" katika kuendeleza uhusiano wa China na nchi za kiarabu katika enzi mpya.

Qin amesema China inapenda kushirikiana na nchi za kiarabu kutekeleza matokeo ya mkutano huo kwa nia ya urafiki kati ya China na nchi za kiarabu na kuharakisha utekelezaji wa mipango minane mikuu ya ushirikiano iliyopendekezwa kwenye mkutano huo, ili kuzinufaisha pande zote mbili. Qin alisema China inaunga mkono Jumuiya ya nchi za kiarabu kwa kubeba jukumu kubwa zaidi katika kukuza amani na utulivu katika Mashariki ya Kati, na nchi za kiarabu kuchunguza kwa kujitegemea njia zao za maendeleo na kutatua masuala ya usalama wa kikanda kupitia ushirikiano na uratibu.

Gheit kwa upande wake amesema kuwa, mkutano wa kwanza wa wakuu wa China na nchi za kiarabu ulikuwa na mafanikio makubwa, na hotuba nzuri ya rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano huo ilipokelewa vyema katika nchi za kiarabu. Nchi za kiarabu ziko tayari kuimarisha mawasiliano na China katika kutekeleza mipango minane mikuu ya ushirikiano mmoja baada ya mwingine.

Gheit pia aliishukuru China kwa kudumisha haki kwa muda mrefu kimataifa, kuunga mkono maendeleo ya nchi za kiarabu na jumuiya ya nchi za kiarabu, na kusaidia nchi za kiarabu kupambana na janga la COVID-19.