Wanawake 50 waliotekwa waendelea kutafutwa Burkina Faso
2023-01-17 09:57:49| CRI

Gavana wa eneo la Sahel nchini Burkina Faso Luteni Kanali Rodolphe Sorgho Jumatatu alitangaza kuwa operesheni ya kuwatafuta wanawake takriban 50 inaendelea, ambao walitekwa nyara na magaidi wiki iliyopita kutoka sehemu mbili zilizoko karibu na mji wa Aribinda mkoani Soum huko eneo la Sahel.

Taarifa iliyotolewa na afisa huyo ilisema katika usiku wa tarehe 12 na 13 Januari, wanawake takriban 50 walitekwa nyara na vikundi vya kigaidi vyenye silaha katika kijiji cha Liki kilichoko umbali wa kilomita takriban 15 kutoka Aribinda, na sehemu nyingine huko magharibi mwa Aribinda.

Alisema wanawake hao walishambuliwa wakati walipotoka kwenda kutafuta matunda. Baada ya taarifa za kupotea kwao kuripotiwa, kazi ya kuwatafuta ikafanyika mara moja.