Uganda yaipongeza China kwa kuziunga mkono nchi za Afrika kwenye utaratibu wa Ushirikiano wa Kusini na Kusini
2023-01-18 10:17:34| CRI

Uganda imeipongeza China kwa kuendelea kuziunga mkono nchi za Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa Ushirikiano wa Kusini na Kusini.

Akiongea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa ngazi ya juu wa Afrika wa Kusini na Kusini na Ushirikiano wa Pande Tatu kwa Maendeleo Endelevu uliofanyika Kampala, Uganda, Makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo amesema China imesaidia nchi za Afrika ikiwemo Uganda kwenye mipango ya maendeleo ya miundombinu ya barabara na nishati.

Alupo amesema kupitia Mfuko wa Mpango wa Ushirikiano wa Kusini na Kusini wa Shirika la Chakula na Kilimo na China, maisha ya Waganda wengi yameboreka kupitia kuongezeka kwa uzalishaji wa kilimo.

Wataalamu wanakutana chini ya kauli mbiu “Kujenga Uwezo wa Kitaifa kwa Kusini na Kusini na Mfumo wa Ikolojia wa Ushirikiano wa Pande Tatu katika Afrika na Kuanzisha Ushirikiano Sawa kwa Jamii Endelevu na Thabiti”.