Mradi wa ukarabati wa reli uliofanywa na kampuni ya China nchini Namibia wakamilika
2023-01-18 13:42:31| cri

Mradi wa ukarabati wa reli kati ya Ghuba ya Walvis hadi Alandis nchini Namibia uliofanywa na Kampuni ya Kundi la Gezhouba la Ujenzi wa Nishati ya China umekamilika.  

Kwa mujibu wa meneja mkuu wa mradi huo Li Jie, mradi huo ulioko kwenye pwani ya magharibi ya Namibia una urefu wa karibu kilomita 110. Kabla ya kufanyiwa ukarabati, reli hiyo ilitumiwa kwa karibu miaka mia moja, na kasi ya treni haikuzidi kilomita 40 kwa saa, na baada ya kufanyiwa ukarabati, kasi ya treni itaweza kufikia kilomita 80 kwa saa.

Naibu Waziri wa Uhandisi na Uchukuzi wa Namibia Veikko Nekundi amesema, mradi huo ni mmoja kati ya miradi muhimu ya Mpango wa Mwaka 2030 wa serikali ya nchi hiyo, na kwamba kukamilika kwake kutaboresha uwezo wa usafirishaji na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa huko.