Iran yataka kuwepo kwa mifumo ya pamoja ya kukabiliana na vikwazo vya upande mmoja
2023-01-19 13:43:55| cri

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Iran Bw. Ali Shamkhani amependekeza kuundwa kwa vyombo vya “pamoja na uratibu” ili kukabiliana na vikwazo vya upande mmoja.

Akiongea mjini Tehran na msaidizi mwandamizi wa Rais wa Russia Bw. Igor Levitin, Bw. Shamkhani ameonya kuwa mfumo wa vikwazo vya upande mmoja unavuruga maendeleo ya nchi zinazolengwa na kuzidisha migogoro ya kieneo na kimataifa. Bw. Shamkhani amesisitiza ulazima wa kutekelezwa kwa miradi ya pamoja ya kiuchumi ndani ya mpango wa mapatano yaliyofikiwa hapo awali kati ya Rais Ebrahim Raisi wa Iran na Rais Vladimir Putin wa Russia.

Bw. Levitin amesema kipaumbele kikuu cha Russia ni kuanza haraka ujenzi wa reli nchini Iran ambayo itaunganishwa na Ukanda wa Kimataifa wa Usafiri wa Kaskazini-Kusini na kukamilisha reli ya Rasht-Astara kwa kuzingatia umuhimu wa kimkakati wa miradi hiyo miwili.