Rwanda yasema DRC imesajili mamluki wa kigeni
2023-01-20 17:57:25| cri

Mvutano wa kidiplomasua kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umeingia katika sura mpya baada ya Rwanda kuituhumu DRC kuhujumu juhudi zinazoendelea za kikanda kuleta utulivu katika sehemu ya mashariki ya nchi hiyo.

Jana alhamis, Rwanda ilidai kuwa DRC inajiandaa kwa vita kwa kuajiri mamluki wa kigeni, na kwamba nchi hiyo inaendelea kutoa silaha na askari wake wanapigana sambamba na makundi yenye silaha mashariki mwa DRC, likiwemo kundi la FDLR.