Rais wa Zanzibar, Tanzania atoa salamu za mwaka mpya wa jadi kwa wachina
2023-01-21 19:15:14| cri

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa watu wote wanaosherehekea mwaka mpya wa jadi wa China, na kusema anawatakiwa mafanikio na ustawi katika mwaka huu wa Sungura.

Rais Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kuhimiza ushirikiano wenye nguvu na China, na kuendelea kutafuta fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizo mbili.