Mashirika ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa yakutana Kenya kuhimiza biashara ya ndani ya Afrika
2023-01-21 17:01:19| cri

Umoja wa Afrika, jumuiya nane za kikanda za Afrika, na wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, wamemaliza mkutano wa siku tatu mjini Nairobi wakijadili namna ya kuhimiza biashara ya ndani ya Afrika.

Mkutano huo umewaleta pamoja zaidi ya wajumbe 150 kujadili njia za ufadhili endelevu wa biashara miongoni mwa nchi za Afrika.

Kwenye ufunguaji wa mkutano huo mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat, amesema kuongeza biashara miongoni mwa nchi za Afrika ni moja ya njia za kuhimiza bara hilo kujitegemea.

Amesema bara la Afrika lina moja ya masoko makubwa zaidi ya biashara huria lenye soko lenye watu bilioni 1.2, linalotarajiwa kuleta njia mpya ya maendeleo.