Mahakama za China zafanya juhudi kuboresha ulinzi wa mazingira ya kiikolojia
2023-01-22 18:23:20| cri

Kwa mujibu wa Mahakama kuu ya Umma ya China SPC, tangu mwaka 2013 kesi zaidi ya 16,000 zinazohusiana na madai ya maslahi ya umma ikiwemo ulinzi wa mazingira, fidia ya uharibifu wa mazingira ya kiikolojia na thibitisho la kisheria zimemalizwa na mahakama kote nchini.

Mahakama kuu imetoa taarifa ikisema mahakama za China siku zote zinahimiza mageuzi ya mfumo wa kisheria kuhusu ulinzi wa mazingira na kuimarisha ushirikiano na waendeshaji mashtaka na idara za utekelezaji wa sheria juu ya ulinzi wa mazingira ya kiikolojia.