Watoto wanane wafariki baada ya boti kupinduka nchini Ghana
2023-01-25 17:05:27| cri

Watoto wanane wa shule katika Mkoa wa Bono Mashariki nchini Ghana walifariki jana baada ya boti iliyokuwa inawapeleka shuleni kupinduka kwenye Ziwa Volta.

Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Majanga (NADMO) liliambia vyombo vya habari kwamba, watoto hao wakiwemo wavulana watano na wasichana watatu wenye umri wa miaka mitano hadi 12, walikuwa miongoni mwa wanafunzi 20 waliokuwa wakielekea shuleni huko Wayokope.

Hivi sasa, kazi za uchunguzi zinaendelea ili kutafuta chanzo cha ajali hiyo.