Kenya yapokea watalii 3,000 wa meli za kitalii ndani ya miezi miwili
2023-01-27 17:53:21| CRI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii ya Kenya Bw. John Ololtuaa amesema kuwa Kenya imepokea watalii 3,000 wa meli za kimataifa za kitalii katika muda wa miezi miwili iliyopita.

Bw. Ololtuaa amesema kuwa Kenya inanufaika na maendeleo ya miundombinu katika kituo kipya cha meli za kitalii kilichoboreshwa katika bandari ya Mombasa ambacho kimesaidia eneo hilo kuingia katika kitengo cha utalii wa meli.

Amebainisha kuwa uendelezaji wa kituo hicho ni muhimu, kwani mashirika mengi zaidi ya meli za kitalii sasa yanalenga Kenya katika ratiba zao.