EAC yatakiwa kupunguza gharama za usafiri wa anga
2023-01-27 17:24:44| cri

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) limezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuwa na Makubaliano ya Pamoja ya Huduma za Usafiri wa Anga na kupunguza gharama za tiketi kwa ndege za abiria na mizigo katika kanda hiyo.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa Jumatano jioni, EABC limesema kwamba miundombinu hafifu, ukosefu wa kanuni sawa na gharama kubwa za usafiri wa anga ni miongoni mwa changamoto zinazoathiri sekta ya usafiri wa anga katika EAC.

Afisa Mtendaji Mkuu wa EABC, John Bosco Kalisa amewataka viongozi wa EAC kukubali kutoa upendeleo wa kitaifa kwa mashirika ya ndege ya EAC, akisema mashirika ya ndege ya kigeni yanapata upendeleo mkubwa kuliko ya EAC.