Polisi wa Tanzania wakamata dhahabu, meno ya tembo
2023-01-30 16:09:52| CRI

Polisi wa Tanzania wamekamata kilo 17.68 za dhahabu na meno sita ya tembo yenye uzito wa kilo 39.34 katika mkoa wa Mara, kaskazini mwa Tanzania.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Tarime-Rorya Geofrey Sarakikya, amesema dhahabu na meno hayo ya tembo yalikamatwa katika msako maalum uliofanyika kati ya Desemba 1, 2022 na Januari 26, 2023. Pia amesema, katika operesheni hiyo, polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama waliteketeza ekari moja ya bangi na kuwakamata watu wanne wanaohusishwa na kulima bangi hiyo kinyume cha sheria.

Kamanda Sarakikya amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na wasimamizi wa sheria katika kubaini vitendo vya uhalifu.