Watu tisa wafariki baada ya basi kuangukiwa na lori huko Lagos, Nigeria
2023-01-30 08:11:29| CRI

Watu tisa wakiwemo watoto wawili, wamefariki dunia baada ya basi lao kuangukiwa na lori huko Lagos, Nigeria.

Mkuu wa Shirika la Kukabiliana na Dharura Jimbo la Lagos (LASEMA), Bw. Olufemi Oke-Osanyintolu, amewaambia wanahabari kuwa ajali hiyo ilitokea kufuatia lori kubwa lililobeba kontena la futi 20 kupoteza udhibiti na kuanguka kutoka kwenye daraja, na kugonga basi moja wakati abiria wanapanda kwenye basi hilo. Jumla ya miili tisa imepatikana kwenye eneo la tukio, na mtu mwingine aliyejeruhiwa ameokolewa na kupelekwa hospitali.