Iran yasema imepata ujumbe kutoka pande husika za makubaliano ya nyuklia kupitia Qatar
2023-01-30 08:36:41| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Hossein Amir-Abdollahian amesema nchi yake imepata ujumbe kutoka pande husika za makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 ikiwemo Marekani kupitia Qatar.

Akishiriki kwenye mkutano wa pamoja na wanahabari na mwenzake wa Qatar Bw. Mohammed bin Abdulrahman Al Thani baada ya mkutano wao huko Tehran, Bw. Hossein Amir-Abdollahian ameshukuru nia nzuri ya Qatar kusaidia kuzileta karibu pande zote katika hatua za mwisho za kufikia mwafaka kuhusu kurejesha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Waziri wa mambo ya nje wa Qatar amesema, Marekani imetoa mfululizo wa ujumbe kwa Qatar ili kuwasilishwa kwa Iran, huku akiongeza kuwa ujumbe huo unahusiana na makubaliano ya nyuklia lakini labda sio wa moja kwa moja.