Mo Dewji apanda kwenye orodha ya matajiri Afrika
2023-02-01 21:08:25| cri

Kwa mujibu wa toleo jipya la Jarida la Forbes, tajiri wa Tanzania Mohammed Dewji, anayejulikana zaidi kama Mo Dewji, amepanda kwenye orodha ya watu matajiri zaidi katika bara la Afrika kutoka nafasi ya 15 hadi nafasi ya 13.

Mfadhili huyo Mtanzania ambaye alitia saini Mkataba mwaka 2016, akiahidi kutoa angalau nusu ya utajiri wake kwa ajili ya misaada, amedumisha utajiri wake unaofikia dola za Marekani bilioni 1.5.

Mkuu huyo wa Mohammed Enterprise Tanzania Ltd (MeTL), alishika nafasi ya 15 katika orodha iliyopita ya Forbes ya mabilionea wa dola barani Afrika, na kuwa bilionea mdogo zaidi barani humo akiwa na umri wa miaka 46.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, Mo Dewji ndiye bilionea pekee Afrika Mashariki aliyeonekana kwenye orodha hiyo. Taarifa zilizotolewa na ofisi yake, inasema mfanyabiashara huyo wa Tanzania alitoa ajira mpya 7,000 na kufanya jumla ya ajira kufikia 35,000 mwaka jana kutoka 28,000 mwaka 2021.