Sauti za Busara baada ya miaka 20 ni hadithi ya zama
2023-02-02 22:21:15| cri

Tamasha la 20 la Sauti za Busara linatarajiwa kutikisa kuta za Ngome Kongwe Zanzibar kwa siku tatu kuanzia tarehe 10 hadi 12 Februari.

Likisifiwa kimataifa kama moja ya matamasha mashuhuri ya muziki barani Afrika, mwaka huu linaadhimisha miaka 20 ya kuonesha muziki bora wa Kiafrika, hatua muhimu ambayo matamasha mengine machache tu ndio yamefanikisha katika Bara la Afrika.

Licha ya changamoto nyingi tangu lilipoanza mwaka 2003, Sauti za Busara limesalia kuwa moja ya siku changamfu kwenye kalenda ya kitamaduni ambazo wadau wake wanazisubiria kwa hamu kila mwaka. Kaulimbiu ya tamasha la mwaka huu ni “Tofauti Zetu, Utajiri Wetu”.