Rais Xi Jinping atoa salamu za pole kwa Rais wa Pakistan kufuatia shambulizi la kigaidi mjini Peshawar
2023-02-02 08:26:17| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pole kwa mwenzake wa Pakistan Arif Alvi, kufuatia shambulizi kubwa la kigaidi lililotokea katika mji wa Pershawar.

Kwenye salamu zake Rais Xi amesema baada ya kupata taarifa kuhusu shambulizi hilo lililosababisha watu wengi kuwa wahanga, kwa niaba ya serikali ya China na watu wake anatoa salamu za rambirambi, na pole kwa waliojeruhiwa na familia zao.

Rais Xi amesema China inapinga aina zote za ugaidi na kulilaani vikali tukio hilo, na kusema China itaendelea kuiunga mkono Pakistan kwenye kutekeleza mpango wake wa kupambana na ugaidi, kulinda utulivu wa jamii na kulinda usalama wa watu.

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang pia ametuma salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Pakistan Bw. Shahbaz Sharif.