Shirika la ndege la Algeria larejesha safari za ndege kati ya Algiers na Beijing
2023-02-02 09:07:55| CRI

Safari za ndege za kawaida kati ya Algiers na Beijing zitarejea kuanzia Februari 19 baada ya kusimamishwa kwa miaka mitatu kutokana na janga la COVID-19.

Shirika la habari la Algeria limemnukuu msemaji wa shirika la ndege la nchi hiyo Amine Andaloussi akisema, safari mbili za ndege kwa wiki kati ya Algiers na Beijing zitarejea kila Alhamis na Jumapili kuanzia Februari 19 mwaka huu.

Andaloussi ameongeza kuwa shirika hilo limetoa bei nafuu ya tiketi zitakazonunuliwa kabla ya Februari 28 kwa ajili ya safari zinazopangwa hadi Oktoba 28.