UNOCHA: Watu karibu milioni 1 wakabiliwa na hatari kubwa ya ugonjwa wa kipindupindu nchini Ethiopia
2023-02-02 09:12:39| CRI

Ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa UNOCHA imesema watu karibu milioni 1 wanakabiliwa na hatari kubwa ya ugonjwa wa kipindupinduu katika wilaya 10 kusini mashariki mwa Ethiopia.

Ofisi hiyo imetoa ripoti mpya ikionya dhidi ya mlipuko wa kipindupindu, wakati idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ikiongezeka hadi 28 nchini humo.

Ofisi hiyo imesema wagonjwa 1,055 wa kipindupindu wameripotiwa, na mlipuko wa kipindupindu unaoendelea umeenea katika maeneo 66 ya wilaya 8 za jimbo la Oromia na wilaya nyingine mbili za jimbo la Somali.