Rais Xi asisitiza juhudi za kuharakisha kuanzishwa kwa muundo mpya wa maendeleo
2023-02-02 08:16:05| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza juhudi za kuharakisha kuanzishwa kwa muundo mpya wa maendeleo na kuimarisha usalama wa maendeleo.

Rais Xi amesema hayo kwenye semina ya pili ya wajumbe wote ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China iliyofanyika Jumanne alasiri hapa Beijing.

Rais Xi amesema kuharakisha kuanzishwa kwa muundo mpya wa maendeleo ni uamuzi wa kimkakati wa kutimiza Lengo la Pili la Miaka 100 na kuhakikisha maendeleo pamoja na usalama, na pia ni mpango wa kimkakati wa kuchukua nafasi nzuri kwenye maendeleo ya siku zijazo.

Rais Xi amesisitiza kuwa ni kwa kuanzishwa haraka muundo mpya wa maendeleo tu, ndipo China itaweza kuimarisha msingi wa uchumi wake na kuhakikisha usalama na utulivu wa maendeleo yake.