China yachangia vitabu vya kiada zaidi ya laki 3 kwa shule za Sudan Kusini
2023-02-02 09:52:24| CRI

Wizara ya elimu na mafunzo ya jumla ya Sudan Kusini imepokea vitabu vya kiada laki 3.3 kutoka kwa serikali ya China kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule za msingi.

Vitabu hivyo vya masomo ya Kiingereza, hisabati na sayansi ni sehemu ya awamu ya pili ya mradi wa ushirikiano wa kiufundi wa elimu nchini Sudan Kusini unaofadhiliwa na China.

Waziri wa elimu wa Sudan Kusini Bw. Awut Deng Acuil ameishukuru China kwa msaada huo, wakati Sudan Kusini iko katika mchakato wa kuunda mfumo wa elimu unaozingatia kujenga ujuzi na uwezo wa wanafunzi katika ngazi tofauti za elimu.

Balozi wa China nchini Sudan Kusini Ma Qiang amesema siku zote sekta ya elimu inapewa kipaumbele kwenye ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.