China yapinga kutumia ushidani kuelezea uhusiano mzima kati ya China na Marekani
2023-02-09 10:05:33| CRI

China imeitaka Marekani kuitazama China kwa njia sahihi na inayofaa, kufuata sera chanya ya kiutendaji kuhusu China, na kushirikiana na China katika kurejesha uhusiano kati ya pande mbili kwenye njia ya utulivu na maendeleo.

Hayo yamesemwa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Mao Ning Jumatano kwenye mkutano na wanahabari alipojibu kauli ya rais Joe Biden wa Marekani alipotoa hotuba ya hali ya taifa bungeni.

Mao alisema China siku zote inaona kuwa uhusiano kati ya China na Marekani si mchezo wa “nipate usipate”, na kusisitiza kuwa mafanikio inayopata upande mmoja ni fursa na sio changamoto kwa upande mwingine, kwani dunia ni kubwa na inaweza kuziwezesha China na Marekani kujiendeleza na kunufaika na kustawi kwa pamoja.

Amesema China haitakuwa na aibu wala kuogopa ushindani, lakini inapinga kutumia ushindani kuelezea uhusiano mzima kati ya China na Marekani. Pia China itashughulikia uhusiano kati ya China na Marekani kwa kufuata kanuni za kuheshimiana, kuishi kwa amani na kunufaishana, na italinda kithabiti mamlaka, usalama na maslahi yake ya maendeleo.