Katibu mkuu wa UM atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa itoe msaada kwa Uturuki na Syria
2023-02-15 18:21:52| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema Umoja wa Mataifa unahitaji dola milioni 397.6 za kimarekani kutoa misaada kwa Uturuki na Syria zinazoathiriwa na tetemeko la ardhi, na ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa itoe misaada. Amesema fedha hizo zitawasaidia watu takriban milioni 5 ndani ya miezi mitatu.

Kwa mujibu wa takwimu za UM, watu milioni 8.8 wa Syria wanaathiriwa na tetemeko la ardhi, majengo zaidi ya 7,400 yameharibika kwa viwango tofauti. Umoja wa Mataifa tarehe 14 ulisafirisha msaada wa kibinadamu kwenye eneo linalodhibitiwa na kundi la waasi nchini Syria kupitia forodha ya Bab Al-Salam ya Syria iliyofunguliwa hivi karibuni.