Rais wa Russia akutana na mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC
2023-02-23 09:27:19| CRI

Rais Vladimir Putin wa Russia jana alikutana na mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Wang Yi mjini Moscow.

Bw. Wang alisema uhusiano kati ya China na Russia umeendelea kuimarika licha ya hali yenye utatanishi ya kimataifa, ambao hausukumwi au kuingiliwa na upande wa tatu.

Pia amesema dunia ya ncha nyingi na demokrasia ya mahusiano ya kimataifa vinavyoungwa mkono na nchi hizo mbili vinaendana na wakati, na kuwa China inapenda kushirikiana na Russia kutoa mchango wa kiujenzi kwa maendeleo na amani ya dunia.

Rais Putin amesema ushirikiano na uratibu kati ya Russia na China umepata mafanikio katika sekta mbalimbali na kuimarisha mafungamano katika mambo ya kimataifa kuna maana kubwa katika kuhimiza demokrasia ya mahusiano ya kimataifa na utulivu wa hali ya dunia.