Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa kuchukua hatua kumaliza pengo la muunganiko
2023-03-09 08:51:01| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuchukua hatua kuondoa pengo la muunganiko, ikiwa ni juhudi za kutimiza fursa za teknolojia na kuendeleza usawa wa jinsia.

Katika hotuba yake iliyosomwa na msaidizi mkuu wa Katibu Mkuu huyo, Courtenay Rattray jana Machi 8 katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Guterres amesema ni lazima kuondoa vikwazo vinavyowazuia wasichana na wanawake kuwa nje ya teknolojia.

Guterres amesema, watu bilioni tatu duniani bado hawajaunganishwa na mtandao wa internet, huku wengi wao wakiwa ni wanawake na wasichana katika nchi zinazoendelea. Amesema wanawake sasa wanachukua chini ya moja ya tatu ya nguvukazi katika maeneo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu, na katika sekta kama akili bandia, ni mtaalamu mmoja kwa watano ndio mwanamke.