China yatoa wito wa kurejeshwa bila masharti kwa misaada ya kiuchumi kwa Sudan
2023-03-21 18:23:18| cri

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amesema, nchi na taasisi husika za kimataifa zinapaswa kurejesha msaada wa kiuchumi kwa Sudan mara moja na bila masharti yoyote.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana, Balozi Dai Bing pia amezitaka pande husika kufanya juhudi katika kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan. Amesema China inatiwa moyo na utayari wa kisiasa na nia ya majadiliano iliyoonyeshwa na pande husika katika mchakato wa kisiasa, na kusema maendeleo yamepatikana katika hali ya kisiasa nchini Sudan.

Ameongeza kuwa, China inaunga mkono pande zote katika kudumisha mchakato wa kisiasa unaoongozwa na kumilikiwa na Wasudan, na kuendelea kwa majadiliano jumuishi, ili kupanua maafikiano na kupata njia ya maendeleo inayoendana na nchi hiyo.