Rais Xi awapa salamu za pole wenzake wa Malawi na Msumbiji kwa kimbunga kikali kilichozikumba nchi hizo
2023-03-23 09:05:15| CRI

Rais Xi Jinping wa China amempa salamu za pole mwenzake wa Malawi Lazarus Chakwera na wa Msumbiji Filipe Nyusi baada ya nchi hizo mbili kukumbwa na kimbuga kikali Freddy.

Kwenye salamu zake alizotoa Jumatatu, Xi alisema amehuzunika kusikia kimbunga hicho kimesababisha vifo na majeruhi wengi na pia mali nyingi kuteketea katika nchi hizo. Kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, alitoa rambirambi zake kwa watu waliofariki kutokana na maafa hayo na kuzipa pole familia na majeruhi. Aidha Xi Jinping amesema anaamini kwamba Malawi na Msumbiji zitashinda janga hilo na kujenga tena nchi zao.