Viongozi wa EAC wapitisha ripoti kuhusu uanachama wa Somalia
2023-06-09 08:55:43| cri

Taarifa iliyotolewa jana na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesema, viongozi wa nchi za EAC wamepitisha ripoti ya ombi la Somalia kuhusu kujiunga na jumuiya hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, ripoti hiyo ilipitishwa kwenye mkutano maalumu wa kilele wa 21 uliofanyika huko Bujumbura nchini Burundi.

Mkutano huo umeliagiza Baraza la mawaziri na Sekretarieti ya EAC waanze kufanya mazungumzo na Somalia, na kuripoti kwenye mkutano ujao wa kawaida wa kilele.