CMG na Kundi la Mediapro wasaini makubaliano ya ushirikiano
2024-07-29 10:13:11| cri

Kundi la CMG la China na kundi la Mediapro la Hispania tarehe 27 yalisaini makubaliano ya ushirikiano huko Barcelona, ambayo yaliafikiana kuhusu ushirikiano kwenye kupeana rasilimali za habari, utengenezaji wa vipindi vya video na sauti na matumizi ya uvumbuzi ya teknolojia mpya. Mkurugenzi wa CMG Bw. Shen Haixiong na mkurugenzi wa kundi la Mediapro Bw. Tatxo Benet walisaini makubaliano hayo kwa niaba ya pande hizo mbili.