Kampuni ya China yakabidhi msaada wa vifaa kwa ajili ya kazi ya kuboresha barabara nchini Ghana
2024-08-01 08:52:51| CRI

Kampuni ya utengenezaji wa mitambo mikubwa ya China LiuGong, imekabidhi zaidi ya vifaa 2,200 vya kazi nzito kwa serikali ya Ghana kusaidia Mpango wa Uboreshaji wa Barabara za Wilaya nchini Ghana (DRlP).

Vifaa hivyo ni pamoja na magreda, matingatinga, mashine za kuchanganya zege, shindilia, malori ya mchana na maboza, vilivyonunuliwa na serikali ya Ghana kwa ajili ya matengenezo ya barabara.

Wakati wa hafla ya makabidhiano Rais Nana Akufo-Addo amesema mradi huo unaashiria hatua muhimu katika harakati za Ghana za maendeleo ya miundombinu. Pia amesema licha ya maendeleo makubwa yaliyopatikana katika maendeleo ya nchi, barabara nyingi, hasa katika wilaya zisizo na uwezo, bado ziko katika hali ya kusikitisha, na kukwamisha shughuli za kiuchumi na juhudi za maendeleo.