Asilimia 40 ya watoto nchini Tanzania hawanyonyeshwi maziwa ya mama
2024-08-02 22:34:08| cri

Asilimia 64 ya watoto nchini Tanzania ndio wanaonyonya maziwa ya mama, hivyo jamii imetakiwa kuungana kwa pamoja katika kutoa elimu kuhusiana na umuhimu wa unyonyeshaji wa watoto kwa ufanisi

Hayo yamesemwa na Daktari bingwa wa watoto kutoka hospitali ya Aga Khan nchini humo, Dk. Mariam Noorani katika maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani. Dk. Mariam ameshauri serikali na taasisi zingine kufanya maboresho katika maeneo ya kazi kwa kuweka sehemu maalum za kunyonyesha.

Naye mtaalamu wa lishe kutoka hospitali hiyo Luiza Tumaini amesema, ni muhimu kuzingatia matumizi ya vyakula vinavyoongeza virutubisho muhimu kwa maziwa ya mama ikiwemo matunda mbogamboga na vyakula vyenye protini ili kulinda madini kwenye mwili na maziwa ya mama.