Msemaji wa serikali ya kijeshi ya Niger Amadou Abdramane Jumanne alitangaza kupitia televisheni ya kitaifa akisema, Niger itavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine “mara moja”.
Kwenye taarifa yake alisema, wanachukua hatua hiyo kutokana na kitendo cha Ukraine cha “kuunga mkono makundi ya kigaidi”, na kutoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya uamuzi juu ya “uvamizi” wa Ukraine.
Siku mbili zilizopita, serikali ya mpito ya Mali ilitangaza kuwa itavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine “mara moja”, kwa kuwa Ukraine imekubali kushiriki kwenye vitendo vya uvamizi dhidi ya Mali.