Muungano wa madaktari usio wa kiserikali umesema kuwa mji mkuu wa Jimbo la Darfur El Fasher, Kaskazini magharibi mwa Sudan umekuwa mahali hatari na pabaya zaidi pa kuishi duniani, kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo.
Kamati ya Awali ya Muungano wa Madaktari wa Sudan imetoa ripoti yake ikisema kuwa wakazi wote wa El Fasher wanawezekana kufariki kutokana na njaa, kiu, risasi, ukosefu wa huduma za afya na matibabu, au madhara mengine ya mzozo unaoendelea.
Kamati hiyo imetoa wito wa kusitishwa mara moja na bila masharti kwa mapigano huko El Fasher, kufungua njia salama ili kuruhusu kuingia kwa misaada ya kibinadamu na matibabu katika mji huo na kuacha kulenga raia na majengo ya kiraia.