Shule saba za Uganda zafungwa katika eneo la magharibi wakati mafuriko yakiwa yameanza
2024-08-08 08:53:17| CRI

Mamlaka ya Uganda imesema takriban shule saba za msingi na sekondari zimefungwa katika wilaya ya magharibi ya Ntoroko kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Akizungumza kwa njia ya simu na Xinhua mkuu wa wilaya ya Ntoroko, Edward Bashungura, alisema mvua hiyo kubwa ilisababisha Mto Semliki na Ziwa Albert iliyopo karibu kufurika kingo, na kusababisha mafuriko, ambapo vijiji 20 vimeathiriwa na shule nyingi kuzama. Bashungura aliongeza kuwa hawakuwa na namna ila kufunga shule kwa ajili ya usalama wa watoto, huku shule nyingi zaidi zikifanyiwa tathmini na kutakiwa kufungwa.

Afisa huyo alisema katika vijiji hivyo pekee, watu 20,000 wameathiriwa na mafuriko. Amebainisha kuwa wanachohitaji sasa ni kurejesha madaraja yaliyosombwa na maji, mahema kwa ajili ya shule, makazi ya wanakijiji walioathirika na vifaa vya kusafisha chakula na maji.

Wiki iliyopita, mamlaka ya hali ya hewa alitangaza kuwa nchi hiyo itakabiliwa na mvua kubwa na radi mwanzoni mwa Agosti.