Polisi nchini Nigeria imesema watu 20 wamefariki baada ya boti ya mbao waliyopanda kulipuka katika mto mmoja mkoani Bayelsa, kusini mwa Nigeria jumatano wiki hii.
Msemaji wa Polisi katika mkoa wa Bayelsa Musa Mohammed amewaambia wanahabari kuwa, boti hiyo iliyokuwa na zaidi ya abiria 64 pamoja na wafanyakazi, ililipuka pembezoni mwa kijiji cha Ezetu 1 katika eneo la Ijaw Kusini. Amesema miili 20 imeokolewa kufuatia operesheni ya uokoaji iliyoanza jumatano, na kwamba zoezi la uokoaji bado linaendelea.
Pia amesema, boti hiyo pia ilikuwa imebeba mazao ya kilimo kutoka kijiji cha Ezetu 1 na ilikuwa ikielekea katika soko la mji mkuu wa Bayelsa, Yenagoa.
Ameongeza kuwa, uchunguzi umeanza kujua chanjo cha mlipuko huo.