Idadi ya vifo kufuatia kuporomoka kwa dampo nchini Uganda yafikia 18
2024-08-12 08:33:50| cri

Idadi ya watu waliofariki kutokana na kuporomoka kwa dampo katika Wilaya ya Kawempe, Kampala, nchini Uganda, jumamosi iliyopita imeongezeka na kufikia 18.

Waziri wa Wizara ya Kudhibiti Maafa na Masuala ya Wakimbizi nchini humo, Bi. Lillian Abel jana alithibitisha kuwa, miili 18 imepatikana hadi sasa, na kuongeza kuwa juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea. Aidha, serikali ya Uganda imetoa chakula na makazi ya muda kwa waathirika na inajaribu kuwahamisha kwenye maeneo ya usalama.