Watu saba wamefariki na wengine 16 kujeruhiwa katika tukio la kukanyagana lililotokea jana kwenye hekalu katika eneo la Jehanabad huko Bihar kaskazini mashariki mwa India.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya India, huenda tukio hilo lilisababishwa na mlundikano wa watu ndani ya hekalu hilo. Polisi wamesema, hali katika eneo la tukio sasa imedhibitiwa na maafisa wa utawala wa eneo hilo wamefika eneo la tukio.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu wameilaani serikali ya eneo hilo kwa kutochukua hatua za kutosha za kukabiliana na idadi kubwa ya watu waliokusanyika kwenye hekalu hilo.