Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer tarehe 12 walitoa taarifa ya pamoja kuhusu suala la Mashariki ya Kati, wakitoa wito wa kupunguza hali ya wasiwasi ya kikanda, na kurejesha mazungumzo mara moja.
Ikulu ya Ufaransa tarehe 12 ilitangaza yaliyomo kwenye taarifa hiyo ya pamoja, ikisema viongozi wa nchi hizo tatu wana wasiwasi kuhusu hali ya eneo la Mashariki ya Kati, wanakubali taarifa ya pamoja iliyotolewa na viongozi wa Qatar, Misri na Marekani, na kutoa wito wa kurejesha mazungumzo mara moja. Taarifa imesema watajitahidi kupunguza hali ya wasiwasi kadri wawezavyo. Taarifa pia imesema “Ni lazima kusitisha vita, mateka wote wanaoshikiliwa na kundi la Hamas lazima waachiwe huru, na watu wa Gaza wapate msaada bila ya vizuizi.”